Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Kikwete amesema ushindi wa Chama cha Mapinduzi – CCM, katika uchaguzi wa 2025 hauna mjadala.
Dkt. Kikwete ameyasema hayo hii leo Januari 19, 2025 wakati akizunguza na wajumbe katika Mkutano Mkuu wa CCM unaoendelea jijini Dodoma.

Amesema, “lakini sio kwa ujanja ujanja ni kwa sababu yapo mambo mengi mazuri yaliyofanywa na serikali zetu mbili, lakini ni mambo ambayo yana manufaa kwa Watanzania.”
Kikwete ameongeza kuwa Wagombea wa vyama vingine watakuwepo, lakini haoni namna wanavyoweza kuishinda CCM.