
Kufuatia sintofahamu iliyojitokeza kati ya wafanyabiashara mkoani Simiyu na mawakala wa vipimo kwa kuwafanyia ukaguzi na kuwapa adhabu pale wanapokuta bidhaa hazina ujazo unaotakiwa mawakala hao wamelazimika kufanya semina kwa lengo la kuwapa uelewa wafanyabiashara juu ya sheria za vipimo.

Sintofahamu hiyo imetokana na kukamatwa pamoja na kupewa adhabu kwa wafanyabiashara kutokana na kupungua ujazo wa bidhaa hali ambayo ilitafsiriwa kama uonevu kwa wafanyabiashara hao wakidai kuwa mhusika wa utengenezaji wa bidhaa na ufungashaji ni kiwanda na si muuzaji kwani wao wanauza kadiri wanavyoletewa
Kufuatia malalamiko yake katibu wa wafanyabiashara hao mkoani Simiyu Kija Mwigulu amesema kuwa kiuhalisia ukimkamata muuzaji unamuonea kwa sababu kitu pekee ambacho mfanyabiashara huangalia ni kuagiza bidhaa na kuuza utengenezwaji na kufungasha ni kazi ya kiwanda
“Mnyororo wa bidhaa unaanzia kiwandani ambako huko ndiko bidhaa hutengenezwa na kupakiwa mimi kama mfanyabiashara nikisha lipia na kutoa oda ya bidhaa kuja dukani kwangu najua kuuza tu”amesema Kija
Kwa upande wake mwenyekiti wa wafanyabiashara hao John Sabu amesema kuwa viwanda ndivyo vinavyosababisha mfanyabiashara aonekane anachakachua bidhaa kwani haiwezekani muuzaji akate inchi moja ya kila nondo kwani hakuna mahali anakwenda kuzitumia
“Hivi kweli nikate inchi moja ya nondo kwanza nitakwenda kuitumia wapi?mnamuacha mtengenezaji ambaye ndiye muhusika namba moja mnakuja kwangu mie naona huu ni mkakati wa kutufilisi na kutufungisha biashara zetu” amesema Sabu.
Sheria ya vipimo namba 340 kifungu namba 26 inamtaka muuzaji kuchunguza bidhaa anayo letewa katika eneo lake la biashara ili endapo mawakala hao watakagua na kuikuta ina mapungufu awe na uthibitisho kuwa vile ilivyo ndivyo ameipokea kutoka kiwanda Fulani ili adhabu ya udanganyifu huo kwa muuzaji akutane nayo mwenye kiwanda kulingana na hiyo sheria
Akitolea ufafanuzi sheria hiyo meneja sheria wakala wa vipimo Oscar Ng’itu amesema kuwa majukumu ya wakala wa vipimo ni kumlinda mlaji ili apate bidhaa inayoendana na thamani ya pesa aliyoitoa kwa mujibu wa sheria ya vipimo.
“Tunawafundisha sheria hizi ili wajue kuwa majukumu yetu ni kumlinda mlaji kwa kuhakikisha anauza bidhaa inayokidhi matakwa ya kisheria na ndiyo maana anakakiwa kukagua bidhaa pale inapomfikia ili ukikutwa na mapunhufu awe na kithibitisho kuwa alivyoletewa ndivyo ilivyo ili sisi tupambane na mletaji wa bidhaa ambaye ni kiwanda”meneja sheria Oscar
Bado elimu juu ya masuala ya vipimo ni changamoto miongoni mwa wafanyabiashara hali ambayo imemlazimu afisa tarafa ya Dutwa Isabela Nyaulingo akimwakilisha mkuu wa wilaya ya Bariadi kuomba ushirikiano uongezwe kati ya watendaji wa serikali na wafanyabiashara sambambana kutoa elimu juu ya vipimo ili kuleta haki na usawa katika utendaji kazi