SINGIDA YATAKIWA KUSHUGHULIKIA CHANGAMOTO MAKUSANYO YA MAPATO KWA WAKATI

Na Saulo Stephen – Singida.

Manispaa ya Singida, imetakiwa kuhakikisha changamoto na taarifa zinazowasilishwa na madiwani kuhusu makusanyo ya mapato katika kata kupitia vikao vya Kamati za Maendeleo ya Kata (WDC) zinafanyiwa kazi kwa wakati ili kuongeza ufanisi wa ukusanyaji wa mapato.

Kauli hiyo imetolewa na Mstahiki Meya wa Manispaa ya Singida,Geoffrey Mdama Kwenye Kikao cha Baraza la Madiwani kilichoketi Agosti 19,2026 kujadili taarifa za maendeleo ya kata ambapo amesema kushughulikia kwa haraka hoja zinazotolewa na madiwani kutasaidia kuondoa vikwazo vinavyoathiri ukusanyaji wa mapato na kuboresha utekelezaji wa shughuli za maendeleo katika kata.

Amesema ushirikiano kati ya viongozi wa kata na Manispaa ni nguzo muhimu katika kuhakikisha changamoto zinazobainishwa kwenye vikao vya WDC zinapatiwa ufumbuzi kwa wakati na kuleta matokeo chanya kwa wananchi.

Katika hatua nyingine, Geoffrey Mdama amewapongeza watumishi waliotunukiwa Tuzo za Utumishi Bora wa Mwezi, akieleza kuwa utaratibu huo ni sehemu ya mkakati wa Manispaa wa kuhamasisha utendaji wenye tija, kuongeza uwajibikaji na kuboresha utoaji wa huduma kwa wananchi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *