SINGIDA MBIONI KUANZA UJENZI WA MIRADI YA KIMKAKATI

Na Saulo Stephen – Singida.

Mkoa wa Singida umeingia mkataba wa mwaka mmoja na nusu na kampuni ya SIHOTECH ENGENEERING LIMITED ,kuanza ujenzi wa miradi ya kimkakati (TACTICS) inayohusisha ujenzi wa soko la vitunguu la kimataifa (MISUNA),Ujenzi wa barabara za ndani, na mtaro wa mvua mnun’guna utakaogharimu jumla ya shilingi Bilioni 24.75.

Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Zainab Katimba akizungumza katika hafla hiyo ya utiaji saini mkataba huo wa kimkakati, amesema mradi huo ni fursa kubwa kwa wanasingida hususani wafanyabiashara wa vitunguu ambao watakwenda kunufaika na ujio wa mradi.

Awali akizungumza katika hafla hiyo Mkuu wa Mkoa wa Singida, Halima Dendego amesema kusainiwa kwa mkataba huo ni habari njema kwa wanasingida, katika kuelekea safari ya upatikanaji wa jiji la Singida ikiwa ni matokeo ya ushirikiano uliopo baina ya viongozi wa serikali, chama na wananchi ndani ya mkoa huo.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Manispaa ya Singida, JoanFeith Kataraia ambae ndie ametia saini kuanza kwa ujenzi huo wa soko la kimataifa la vitunguu Misuna, amesema atahahakikisha anasimamia kikamilifu ili mradi huo uweze kukamilika kwa wakati na kwa mujibu wa makubaliano waliyoingia na kampuni hiyo ya wakandarasi ili kuwanufaisha wafanyabiashara wa vitunguu na wananchi kwa ujumla katika manispaa ya Singida.

Kwa upande wao baadhi ya wafanyabiashara wa vitunguu kutoka soko la vitunguu misuna, akiwemo mwenyekiti wa Soko hilo Iddi Swalehe Mwanja wakizungumza na jambo fm wameelezea namna walivyopokea ujio wa mradi huo wakiamini kwamba utaendana na hadhi ya uzalishaji wa zao hilo mkoani Singida.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *