SINGIDA KUWA KITOVU UTOAJI HUDUMA BORA ZA AFYA KANDA YA KATI

Na Saulo Stephen – Singida.

Mkoa wa Singida unaendelea kuimarisha sekta ya afya kwa lengo la kuwa kitovu cha utoaji wa huduma bora za afya katika Kanda ya Kati, sambamba na kutekeleza dira ya maendeleo ya Taifa kuelekea mwaka 2050.

Akizungumza kuhusu maboresho hayo, Mganga Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dkt. Jesca Lebba, amesema juhudi zinaendelea katika ujenzi na ukarabati wa hospitali, vituo vya afya na zahanati, pamoja na kuimarisha miundombinu, watumishi, huduma za mkoba, huduma za kibingwa na upatikanaji wa vifaa tiba.

Amesema hatua zilizopigwa zimewezesha baadhi ya huduma ambazo awali wananchi walilazimika kuzifuata nje ya Mkoa, ikiwemo huduma za kibingwa, upasuaji na huduma za uzazi, kupatikana sasa ndani ya Singida. “Lengo letu ni kuhakikisha mwananchi wa Singida hapati sababu ya kusafiri mbali kutafuta huduma ambayo anaweza kuipata hapa hapa ndani ya Mkoa,” amesema Dkt. Lebba.

Aidha, amesema Serikali inaendelea kuboresha upatikanaji wa vifaa tiba na dawa, huku Mkoa ukiimarisha huduma za afya ya mama na mtoto pamoja na mapambano dhidi ya magonjwa yasiyoambukiza na ya kuambukiza, ikiwemo malaria, TB na HIV/AIDS.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *