Klabu ya Singida Fountain Gate FC imethibitisha kumteua mkufunzi Ernst Middendorp (64) raia wa Ujerumani kuwa kocha mkuu klabuni hapo kuchukua nafasi ya Mholanzi Hans van der Pluijm (74) aliyebwaga manyanga.
Middendorp amewahi kuinoa klabu ya FC Augsburg inayoshiriki ligi kuu nchini Ujerumani (BUNDESLIGA), lakini pia vilabu kama Arminia Bielefeld na VfL Bochum za Bundesliga.
Kwa Afrika amewahi kuzifunza timu za Chippa United, Saint George, Kaizer Chiefs, Swallows FC, Maritzburg United, Asante Kotoko FC na nyinginezo.