Na Gideon Gregory,Dodoma
Sekretarieti ya maadili ya viongozi wa umma imemfikisha mbele ya Baraza la madili kwa viongozi wa Umma leo Jijini Dodoma Mkuu wa Wilaya Ya Tanganyika Mkoa wa Katavi Onesmo Buswelu kwa tuhuma za kukiuka maadili ya viongozi wa umma ambapo anatajwa kutumia lugha chafu za matusi kwa baadhi ya watumishi na kutumia madaraka yake vibaya ya kumuweka mtu mahabusu bila kufuata utaratibu.
Mbele ya baraza kiongozi huyo kutoka wilaya ya Tanganyika amesikiliza shauri lake kutoka kwa uwakilishi wa serikali pamoja na mashahidi watatu waliotoa ushahidi dhidi yake.
Baada ya kusikiliza shauri hilo alipewa nafasi ya kujitetea ambapo amekana tuhuma dhidi yake huku akisema yeye amekuwa mbuzi wa kafara kwa baadhi ya maofisa wasio waaminifu katika kazi ya kupigania miradi ni ngumu wilayani humo.
Baraza lililosikiliza shauri hilo linatarajiwa kuktana tena Juni 7,2024 ili kutoa ushauri kwa mamlaka juu ya tuhuma zinazomkabili.
Katika kuhakikisha Watumishi Serikalini wanatenda haki katika sehemu zao mbalimbali za kazi ili kutoa huduma bora kwa wananchi Serikali ilitunga sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma Namba 13 ya mwaka 1995,utngwaji wa sharia hiyo ulipelekea kuanzishwa kwa baraza Tume ya maadili na baraza lengo ikiwa ni kusikilizwa kwa mashauri mbalimbali yanayohusu viongozi.