SIMBA YAVUNA MILIONI 20 ZA RAIS SAMIA

Wawakilishi pekee wa Tanzania katika michuano ya Kombe la Shirikisho, Simba SC, imeondoka na zawadi nono ya Goli la Mama ya Sh Milioni 20 kutoka kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Fedha hizo zimetokana na timu hiyo ya Tanzania kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya wageni wao Stellenbosch wa nchini Afrika Kusini.

Fedha hizo za goli la Mama zimepokewa na nahodha wa Simba, Mohamed Hussein, dakika chache baada ya mchezo huo kukamilika katika Uwanja wa Aman, mjini Zanzibar.

Hussein alitumia muda huo kumshukuru Rais Samia kwa kuwazawadia kiasi hicho cha pesa kutokana na ushindi wao, wakiamini kuwa zitaongeza hamasa katika mechi ya marudiano ya Kombe la Shirikisho, mchezo utakaochezwa nchini Afrika Kusini.

Rais Samia anajulikana kama mkombozi namba moja kwenye sekta ya michezo hususan mpira wa miguu baada ya kuanzisha hamasa ya kuzawadia fedha za goli la Mama timu zinazoshiriki michuano ya Kimataifa, ambapo timu mbalimbali kama vile Yanga, Azam nk.

#GoliLaMama

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *