Timu ya Simba imefanikiwa kumfunga CS Sfaxien goli 1 – 0 kwenye mchezo wao wa Kombe la Shirikisho ambapo baada ya matokeo ya leo, Simba anaongoza kundi lake kwa kuwa na point 9.
Msimamo wa kundi uko hivi.
Baada ya mchezo kukamilika, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan awaandikia Simba baada ya ushindi wao ambapo amesema ‘Hongera kwa Klabu ya Simba kwa ushindi kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika (CAF Confederation Cup) dhidi ya CS Sfaxien’ – Rais Samia.
‘Mmewapa mashabiki na Watanzania wote kwa ujumla burudani na furaha. Endeleeni kuweka juhudi na kuipeperusha vyema bendera ya nchi yetu kimataifa, mkitumia mazingira bora ya kufanya vyema kwenye michezo tunayoendelea kuyaboresha siku baada ya siku. Ninawatakia kila la kheri katika michezo iliyosalia.’ – Rais Samia.