Klabu ya Simba baada ya kupata barua ya kufungiwa mashabiki mechi moja na shirikisho la soka Afrika (CAF) leo wametangaza kampeni maalum ya mashabiki ambao watachangia kama sehemu ya kuwajibika na ile adhabu.
Meneja wa mawasiliano ya Simba Ahmed Ally amesema “Tumekuja na kampeni maalumu ambayo hii imeombwa na amshabiki wenyewe wakitaka kuwajibika baada ya kufanya makosa yale. Tumewaletea mfumo wa kuchangia ili kitakachopatikana twende tukalipe faini na Simba Sports Club ibaki salama. Kampeni hiyo tumeipa jina la TUNAWAJIBIKA PAMOJA.” – Ahmed Ally.
“Natoa rai kwa Wanasimba, asijekutokea Mwanasimba wa kuchangisha kwamba kikifika kiasi fulani tutapeleka ofisini. Kila Mwanasimba atume fedha yake moja kwa moja kwenye namba ya ofisi ambayo imetolewa.” – Ahmed Ally.
“Zoezi letu tumeliweka kwa muda sio kwa kiwango kwahiyo kama ikifika milioni 100 na muda bado tutawaachia. Wanasimba wanapaswa kuonyesha nguvu yao, wanapaswa kusimama na timu yao.”- Ahmed Ally.