Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, George Simbachawene amesema kama Klabu ya Simba inaamini kupoteza kwa magoli 5-1 dhidi ya Yanga kumechangiwa na mazingira ya Rushwa basi taarifa hiyo ikaripotiwe Ofisi ya TAKUKURU Temeke, Dar es Salaam.
Awali, Mbunge Festo Sanga alihoji mpango wa Serikali kukabiliana na Rushwa michezoni baada ya kuwa na tetesi za madai ya Rushwa katika mchezo huo uliopigwa kwenye Uwanja wa Mkapa.