SIMBA WAANGUKIA PUA SHAURI LA DAMARO CAMARA

Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF),
imetupa shauri la klabu ya Simba kuhusu uhalali wa mchezaji Mohamed Damaro Camara.

Taarifa ya TFF iliyotolewa hii leo Aprili 2, 2026 imeeleza kuwa, Simba iliwasilisha malalamiko mbele ya Kamati hiyo ikipinga uhalali wa usajili wa Camara, kwa madai unaifanya Yanga kuwa na wachezaji 13 wa kigeni badala ya 12.

Damaro Camara.

Klabu hiyo ilidai usajili wake umekiuka Kanuni ya 62(1) ya Ligi Kuu pamoja na Kanuni za
Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA).

Kamati katika uamuzi wake, ilisema usajili wa Camara hauna dosari kwa vile habanwi na
Kanuni zilizowasilishwa na klabu ya Simba na kwamba uamuzi kamili wa shauri hilo utatumwa kwa Mlalamikaji.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *