Simba Uwanjani leo Ligi ya Mabingwa Afrika

Klabu ya Simba itashuka dimbani usiku wa leo Februari 23, 2024 dhidi ASEC Mimosas ya Ivory Coast katika mchezo wa raundi ya pili Ligi ya Mabingwa Afrika.

Mchezo huo utachezwa katika Uwanja wa Félix Houphouët-Boigny jijini Abidjan saa 4:00 usiku, huku Simba akihitaji ushindi kwa udi na uvumba.

Simba ambayo ipo nafasi ya pili baada ya mechi nne ina na pointi tano katika msimamo wa kundi B lenye timu za Jwaneng Galaxy, Wydad Casablanca na vinara ASEC.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *