Simba SC watambulisha winga wa ASEC

Simba SC wamemtambulisha Winga wa ASEC Mimosa raia wa Ivory Coast Aubin Kramo.

Winga huyu mwenye umri wa miaka 27 ametua Msimbazi kwa mkataba wa miaka miwili.

Aubin anatumia miguu yote kwa uhakika tena bila kupepesa ana kitu anachoweza kuchangia kwenye kikosi cha Mbrazil Robartinho.

Simba wana kumbukumbu mbaya sana mbele ya miguu ya huyu kijana kwani Machi 20, 2022 aliwafunga Msimbazi kwenye hatua ya Makundi wakiwa kwao na mchezo kumalizika kwa Asec Mimosa 3-0.

Comments are closed.