Simba SC watakiwa kuomba radhi kwa hili

Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) kwa kushirikiana na Chama Cha Watu wenye Ualbino Tanzania (TAS) leo agosti 09, 2023 kimelaani vikali kitendo kilichofanywa tarehe 6/08/2023 siku ya Simba day kumtumia mtu mwenye ualbino mithili ya mtu aliyekua katika hali ya nusu utupu na aliyevaa nepi ya mkojo jukwaani mbele va kadamnasi ya maelfu kwenye uwanja wa taifa.

Aidha LHRC imetanabaisha tukio hilo linafuatia tukio jingine lililofanywa na timu hiyo mwaka jana tarehe 8/8/2022 siku ya Simba day ambapo kulitokea kitendo cha kutumia jeneza, msalaba na kumnasibu mtu mwenye albino kama msukule. kupitia mkutano wa LHRC, tas na vyombo vya habari wamebainisha kuwa vitendo hivyo vinatweza utu wa watu wenye albino nchini na vinapelekea kuwepo kwa mijadala mingi katika jamii ikiwemo mitandaoni inayoonesha dhihaka kwa watu wenye albino kinyume na haki za binadamu.

“Tunautaka uongozi wa Simba uombe radhi kwa watu wenye ualbino na umma wa watanzania kwa vitendo hivi vya kutweza utu wa watu wenye Albino, na tunaiomba Serikali na TFF wasimamie jambo hili,” Taarifa ya LHRC na TAS

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *