Simba SC kutumia uwanja wa Chamanzi

Bodi ya Ligi Kuu Tanzania imesitisha matumizi ya uwanja wa Jamhuri uliopo mjini Morogoro kwa michezo ya Ligi Kuu ya NBC kutokana na mapungufu kadhaa kwenye miundombinu ya uwanja inayosaidia urushaji wa matangazo mbashara ya runinga.

Hivyo Klabu ya Simba ambayo ilikuwa ikiutumia uwanja huo kwa michezo yake ya nyumbani kwa sasa itatumia uwanja wa Azam Complex uliopo Dar es Salaam kwa michezo yake ya nyumbani.

Taarifa ya Bodi imetolewa jioni hii wakati Simba SC ikiwa Tanga Mkwakwani ikicheza na Coastal Union

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *