Klabu ya Simba SC imeangukia pua msimu huu baada ya kumaliza nafasi ya tatu na kukata tiketi ya kushiriki kombe la Shirikisho Afrika msimu ujao huku Azam FC ikiungana na Yanga SC kucheza Ligi ya Mabingwa Afrika msimu ujao.
Kwenye mbio za ufungaji bora, Stephanie Aziz Ki amejihakikishia kiatu cha ufungaji bora baada ya kufunga hat-trick na kufikisha magoli 21 kwenye Ligi Kuu ya NBC Tanzania bara msimu huu, mawili mbele ya Faisal Salum ‘Feitoto’ mwenye magoli 19.
Kwenye mbio za kuwania tuzo ya kipa bora wa msimu, Ley Matampi wa Coastal Union amempiku Djigui Diarra wa Yanga Kwa kufikisha ‘clean sheets’ 15 baada ya kuisaidia Coastal Union kwenye sare ya 0-0 dhidi ya KMC.
FT: Simba 2-0 JKT Tanzania
⚽️ Saido (P) 88′
⚽️ Onana 90+3′
FT: Yanga 4-1 TZ Prisons
⚽️⚽️⚽️ Aziz Ki 11’, 12’, 79’
⚽️ Musonda 52’
⚽️ Ngassa 5’)
FT: Geita Gold 0-2 Azam Fc
⚽️ Yeison 58’
⚽️ Feisal 71’
FT: Namungo 3-1 Tabora United (Buswita 19’, 28’p, Manyanya 77’ / Abbas 84’)
FT: Coastal Union 0-0 KMC
FT: Mashujaa 3-0 Dodoma Jiji (Lusajo 6’, 47’, Ulomi
FT: Ihefu SC 5-1 Mtibwa Sugar (Bola 5’, Chukwu 16’, Mgunda 41’, 62’, 74’ / Karihe 37’)
FT: Singida FG 2-3 Kagera Sugar (Kidemile 19’, Kaseke 84’p / Mafie 40’, Mbaraka 46’, Mhilu 82′