Klabu ya Soka ya Simba SC leo kupitia Afisa Habari wake Ahmed Ally imemtangaza Misso Misondo na Wazee wa Makoti kuwa watatoa burudani kwenye uzinduzi wa hamasa ifikapo Disemba ,16 Mbagala Zakhem, hii ni kuelekea Mchezo wao wa Marudiano wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Wydad Athletic Club siku ya Jumanne.
“Jumamosi naomba Wanasimba mjitokeze kwa wingi mje mpate show ya Miso Misondo. Wale wazee wa kucheza hiyo siku mtawaona vizuri na Ijumaa tutaachia remix kwa ajili ya Simba.Naishukuru Simba kwa kunipa nafasi hii, nilikuwa natamani siku moja kufanya kazi na klabu hii.”- Miso Misondo.