Mchezo wa kwanza na wafunguzi wa michuano ya African Football League, umechezwa dimba la Mkapa, jijini Dar Es Salaam na umetamatika kwa timu zote kutoshana nguvu kwa kufungana goli mbili.
Al Ahly ndio walioanza kuona lango la simba kipindi cha mwanzo ambapo goli limefungwa na Reda Slim dakika ya 45+3 mchezaji huyo amesajiliwa kutoka FAR Rabat kwa Euro 2.0M (Bilioni 5+).
Kipindi cha pili dakika ya 53 na 67 Simba walifanikiwa kupata goli mbili kutoka kwa Kibu Denis na Sadio Kanoute.
Hata hivyo dakika chache baadae Al Ahly waliweza kusawazisha kwa kupata goli la pili.
.
2 responses to “Simba na Al Ahly watoshana nguvu”
Mchezo ulimalizika je ?
sare