Klabu ya Simba SC imetangaza kucheza na mabingwa wa ligi kuu soka nchini Zambia timu ya Power Dynamos, kwenye kilele cha wiki ya Simba (SIMBA DAY), Agosti 6, 2023 kwenye uwanja wa taifa Dar es salaam.
Power Dynamos itaiwakilisha Zambia kwenye ligi ya mabingwa barani Afrika msimu wa 2023/24, baada ya kumaliza kinara ikiwa na alama 65 kwenye mechi 34.