SIMANIENI KIKAMILIFU UTEKELEZAJI WA SERA, MITAALA MIPYA YA ELIMU – RAIS SAMIA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan ameitaka Wizara ya Fedha, Wizara ya Mipango na Uwekezaji, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia na Ofisi ya Rais-TAMISEMI, kuwezesha na kusimamia kikamilifu utekelezaji wa Sera na Mitaala mipya ya Elimu, ili ilete matokeo yaliyokusudiwa katika kuimarisha sektaya elimu.

Rais Dkt. Samia ametoa tamko hilo leo Febriari 1, wakati wa hafla ya uzinduzi wa Sera ya Elimu naMafunzo ya 2014 Toleo la Mwaka 2023 iliyofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Mrisho Kikwete.

Amesema, mabadiliko na kukua kwa kasi kwa Teknolojia ya Habari naMawasiliano (TEHAMA) kunaweza kuwa na mchango chanya au hasi kutokana na namnajamii itakavyojipanga, hivyo ili kuendana na mabadiliko hayo ni lazima kutumia TEHAMA kutoa elimu kwa urahisi na kuwandaa vijana wetu kuwa na taaluma na ujuzi wa taalumazinazoenda na mageuzi ya TEHAMA bila kuathiri maadili ya vijana hao.

Vile vile, Rais Dkt. Samia amesema Serikali haina budi kuwa na maandalizi ya kutosha kwakuinua viwango vya ubora wa elimu, na kuwandaa vijana vizuri zaidi ili waweze kumudu stadi muhimu zitakazowawezesha kuajiriwa na kujiajiri pamoja na kuwajengea ujasiri nakuweza kujiamini.

Rais Dkt. Samia pia amesema dhamira ya kufanya mabadiliko katika Sera ni kumuandaa kijana anayejiamini na mwenye nyenzo stahiki za kukabiliana na ushindani wa kikanda nakimataifa ili, kwa kutumia utajiri wa rasilimali zetu, aweze kunufaika kiuchumi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *