SIMAMIENI PESA ZA SERIKALI ZIRUDI KWA WAKATI – KATIBU TAWALA SINGIDA.

Na Saulo Stephen-Singida. 

Maafisa Maendeleo ya Jamii katika Halmashauri ya Manispaa ya Singida, Mkoani Singida wametakiwa kuhakikisha wanasimamia Fedha zilizokopeshwa kwenye Vikundi vilivyo katika maeneo yao,zinarejeshwa kwa Wakati.

Hayo yamesemwa na Dkt.Fatuma Mganga,ambe ni katibu tawala mkoa wa Singida wakatia akizungumza na maafisa maendeleo ya jamii kutoka Manispaa ya Singida, kwenye kikao kazi kilichowakutanisha ,maafisa maendeleo ya,katibu tawala pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Singida,ambapo Dkt.Fatuma amewataka maafisa hao kujitahimini katika utendaji wao.

Amebainisha kuwa kila afisa maendeleo ya jamii anapaswa kujitahimini katika eneo lake kwa kusimamia shughuli mbalimbali ambazo zinahusiana na Maendeleo ili kutimiza malengo katika uwajibikaji.

Awali akifungua kikao hicho Mkuu wa Mkoa wa Singida Halima Omari Dendego, amesema kuwa kuwa afisa maendeleo anatakiwa kuwajibika katika kila sekta iliyopo kwenye eneo lake.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *