Silaha na risasi 12 zakutwa choo cha shule

Jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga limefanikiwa kukamata silaha aina ya Pistol Browining ikiwa na risasi 12 ambayo ilikuwa imetelekezwa chooni katika shule ya Savana iliyopo katika kata ya Ibadakuli Halimashauri Ya Manispaa Ya Shinyanga.

Akitoa taarifa kwa vyombo vya habari juu ya mwenendo wa jeshi hilo katika kipindi cha mwezi mmoja uliopita kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga Acp Janeth Magomi amesma kukamatwa kwa silaha hiyo kumetokana na ushirikiano mwema kati ya jeshi hilo na jamii ambapo wananchi waliweza kutoa taarifa kuhusu silaha hiyo.

Akizungumzia utayari wa jeshi hilo katika kipindi cha kuelekea sikukuu za krismasi na mwaka mpya kamanda Magomi amesema watakabiliana na vitendo mbalimbali vya kihalifu ili kulinda usalama wa raia na mali zao huku akianisha kuwa wameendela na doria na misako katika maeneo yote ya shinyanga ili kubaini wahalifu kwa kushirikiana na vikundi vya ulinzi shirikishi.

Aidha kamanda Magomi mezungumzia pia mafaniko ya jeshi hilo katika kukabiliana na uhalifu ambapo wameweza kukamata jumla ya gramu 2205 pamoja na kete 61 za dawa za kulevya aina ya bangi pamoja na pikpiki 11 pamoja na vifaa vya ujenzi vilivyokuwa vimeibiwa katika mradi wa ujenzi wa nyumba za wahanga wa kubomoka kwa bwawa la maji tope la mgodi wa alimasi wa Mwadui.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *