Categories

Do you have a Story?

Call us on 0677 644 444 to submit your news story or incident report!

Sikujua kama wamemnyima kolabo Diamond

Rapa Frasha, memba wa kundi la P-Unit, kutoka Kenya, amedai kuwa hakujua kama wenzake waliichomoa kolabo na Diamond Platnumz. Amesema hayo wakati wa mahojiano na Nairobi News siku ya jana (Novemba 8).

“Sikuwa najua kama waliikata kolabo na Diamond, lakini katika kujenga brand unapaswa kuwa mwangalifu sana unayefanya naye kazi. Nina hakika hata yeye ana watu ambao hawezi kushirikiana nao kwa sasa kutokana na nafasi yake ya sasa,” ameongea Frasha.

Hivi karibuni mmoja wa memba wa kundi hilo Bon’Eye, alisema walimnyima kolabo Diamond Platnumz enzi zao wako noma na walimkalisha hotelini saa 4 kwa kuwa alikuwa amepauka sana.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *