SIKU YA WAZEE DUNIANI: JAMII ITEKELEZE MATAKWA, MAHITAJI YAO KIKAMILIFU

Maadhimisho ya siku ya Wazee duniani hufanyika Oktoba Mosi ya kila Mwaka, baada ya Desemba 14, 1990 Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kuitaja tarehe hiyo kuwa Siku ya Kimataifa ya Wazee.

Baadaye mwaka 1991, Baraza Kuu lilipitisha Kanuni za Umoja wa Mataifa kwa Wazee ambapo lengo la siku hiyo ni kuelimisha jamii haki na stahili mbalimbali zinazohitajika kwa wazee hao sanjari na kuwakumbusha wazee umuhimu wa uwepo wao katika jamii husika.

Sote tunafahamu kwamba ukuaji wa haraka wa idadi ya watu wanaofanya uwepo wa ongezeko la uzee, unasisitiza umuhimu wa kukuza afya, kuzuia, na kutibu magonjwa katika kipindi chote cha maisha.

Sina shaka pia kwa pamoja, sote tunatambua kwamba jukumu la kumtunza mzee, linakwenda sambamba na kumhudumia, pindi anapoumwa na anapokuwa mzima.

Hivyo, Jambo FM inaona upo umuhimu na inasisitiza kwamba, famila na jamii kwa ujumla, wote wana wajibu na jukumu la kuwatunza wazee, ikiwemo kuwaheshimu na kutekeleza matakwa ya mahitaji yao kikamilifu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *