ALIINGIA ICU JANUARI 24
Katika verse ya kwanza kwenye ngoma mpya ya Profesa Jay ya Siku 462, ameweka wazi kwamba Januari 24, 2022, alilazwa katika Chumba cha wagonjwa mahututi (ICU), Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.
MWILI ULIJAA UCHAFU IKABIDI ATOBOLEWE KOO
Profesa Jay anaendelea kusimulia kwenye verse ya pili, kuwa ilibidi atobolewe koo baada ya hali yake kuwa mbaya hasa baada ya kuzidiwa uchafu mwilini .
KUZUSHIWA KIFO
Hii ni verse ya tatu na ya mwisho kwenye ngoma ya Siku 462 ambapo Jay anasimuia namna ambayo kuwa kuna watu walichukua Clip na picha akiwa yupo ICU na zikafanya azungumziwe sana ikiwemo kuzushiwa kufa. Kufuatia maradhi haya Jay kwasasa amesema anamjua Mungu kiroho na Kimwili.