SIASA: KWA MTINDO HUU KUNA MKONO WA MTU SI BURE

Vyama vya upinzani Barani Afrika, vinaweza kuendelea kuzaliwa na kuwepo kwa muda mrefu katika siasa, lakini itavichukua muda mrefu kufanikisha kile ambacho wanahitaji kutokana na baadhi ya Wanasiasa wake kuingia katika migogoro ya ndani na kuishia kufarakana.

Bado haifahamiki kama wanarubuniwa na Vyama Tawala kutengeneza mizozo ya ndani, ama wanapishana kauli kutokana na mambo ya kisera na uwajibikaji wao.

Ushahidi upo, mfano chini Zimbabwe, Nelson Chamisa aliachana na Chama chake akitoa sababu mbalimbali ambazo zinaacha maswali, huku Nchini Burundi, Agathon Rwassa akifukuzwa kwenye chama chake.

Huko Uganda, mzozo uliwahi kufukuta ndani ya Chama cha Mwanasiasa maarufu Bob Wine na kilichokuwa chama cha Kizza Besigye cha FDC nacho kikagawanyika na hapa Tanzania mambo si haba kila uchao jipya halikosenani.

Kwa kumbukumbu ni kwamba hapa mwaka 2020 uchaguzi mwezi Oktoba mara tu baada ya kumalizika, aliyekuwa mgombea Urais wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu alitangaza kwamba maisha yake yako hatarini na akaamua kuondoka kwenda kutafuta hifadhi ya kisiasa ughaibuni.

Moise Katumbi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) na baadhi ya waliokuwa wapinzani wa Rais aliyepita wa nchi hiyo, Joseph Kabila nao waliwahi kukimbia taifa lao wakihofia usalama wao.

Bob Wine.

Wiki moja baada ya Yoweri Kaguta Museveni kutangazwa mshindi wa uchaguzi mkuu wa Uganda, mpinzania wake Mkuu Robert Kyagulanyi maarufu kama Bobi Wine, naye alipambani, ili kuachiwa huru katika kifungo cha nyumbani.

Kinachotokea katika siasa za Afrika Mashariki kwa sasa pia kinaakisi kinachoendelea katika mataifa mengi duniani, yakiwemo yale yaliyoendelea ambako mfumo wa kidemokrasia ulioanza kumea duniani kuanzia miaka ya 1990 una changamoto.

Mfumo wa kuongoza dunia (World Order), uliowekwa na mataifa makubwa baada ya kumalizika kwa Vita ya Pili ya Dunia, umeanza kutikiswa na kwa kuwa wakubwa wenyewe wanapiga chafya, nchi za Afrika na katika muktadha huu, nchi za Afrika Mashariki, zimeanza nazo kupata msuguano.

Moise Katumbi.

Mojawapo ya sababu zinazosababisha kinachoendelea katika nchi nyingi za Afrika Mashariki, ni ukosefu wa Katiba zinazotoa nguvu na mamlaka kwa vyombo vya uwajibikaji na utoaji haki.

Kkwa mfano Katiba mpya ya Kenya imeweka utaratibu mzuri wa namna ya kuwapata majaji wa Mahakama Kuu na ya Juu, Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama na wizara nyingine nyeti na hivyo wananchi na serikali imeanza kufahamu kwamba hakuna aliye juu ya sheria.

Tundu Lissu.

Kama taasisi za uwajibikaji na utoaji haki hazitafanyiwa mabadiliko na kama mfumo wa uendeshaji wa dunia hautabadilika na upepo kutoka kwa utawala mpya wa Biden, upepo uliotabiriwa kubaki kwa muda mrefu zaidi ingawa tayari Trump katia shubiri.

Swali kuu ni je, nani yupo nyuma ya migogoro hii, na ni ipi sababu hasa ya kuleta migongano inayosababisha mifarakano isiyo na tija kwa Vyama vinavyopambania maslahi yake, ya Umma na maendeleo ya Taifa?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *