Categories

Do you have a Story?

Call us on 0677 644 444 to submit your news story or incident report!

Shule ya Msingi Ibadakuli B Shinyanga yakamilika kwa shilingi milioni 561

Mwalimu mkuu wa shule ya Msingi Ibadakuli B iliyopo Manispaa ya Shinyanga Bi.Tunzayamungu Iddy amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kuwezesha ujenzi wa shule hiyo iliyogharimu kiasi cha shilingi milioni 561 kupitia mradi wa Boost.

Akizungumza na Jambo Fm kupitia mahojiano maalum hivi karibuni,Mwalimu Tunza ameeleza kwamba ongezeko kubwa la wanafunzi pamoja na uchache wa miundombinu katika shule ya msingi Ibadakuli ni sababu zilizopelekea kujengwa kwa shule hiyo yenye jumla ya vyumba 14, jengo la utawala, matundu ya vyoo 16,darasa la awali lenye vyumba viwili.

Baada ya kukamilika kwa ujenzi wa shule husika, Sospeter Swagi na Maria John Kapela ambao ni baadhi ya wazazi wa wanafunzi wanaosoma katika shule hiyo wameeleza kuwa kwa kutambua umuhimu wa elimu kwa watoto wao,wazazi wameshiriki katika kuhakikisha watoto wanapata chakula wakiwa shule,malipo ya mlinzi wa shule pamoja na kuhakikisha miundombinu ya shule inalindwa ipasavyo.

Baadhi ya wanafunzi wanaosoma katika shule hiyo wameishukuru serikali kwa kuwezesha kukamilika kwa ujenzi wa shule hiyo hali waliyoelezea kwamba imepunguza utoro,kuamsha ari ya kupenda elimu kutokana na uwepo wa miundombinu rafiki na idad iya kutosha ya waalimu wa masomo yote.

Lakini licha ya kukamilika kwa shule ya msingi Ibadakuli B bado kuna changamoto zinazoikabili ukosefu wa nishati ya umeme pamoja na vifaa muhimu vya kofisi na tanki la kuhifadhia maji hali inayomlazimu mwalimu mkuu wa shule hiyo Tunzayamungu Iddy na kuwaomba wadau wa maendeleo mkoani Shinyanga kuwasaidia kuzitatua changamoto hizo.

Kwa upande wa elimu,Mkoa wa Shinyanga umejenga Shule za Msingi mpya 9 , madarasa 84 na matundu ya vyoo 133 ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa mradi wa Boost na kukamilika kwa shule ya Msingi Ibadakuli kumewezesha kupatikana kwa miundombinu rafiki ya elimu ambapo hadi sasa kuna vyumba vine vya ziada vinavyoshubiri wanafunzi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *