Na Saulo Stephen – Singida.
Jumla ya shule tatu mpya za Sekondari Mufumbu,Mwankonko na Dkt. Salmin zilizogharim kiasi cha Shilingi milioni 616 zilizopo katika Halmashauri ya Manispaa ya Singida zinatarajia kuanza kupokea wanafunzi wa kidato cha tano kuanzia Mwezi Julai 2025.
Shule ya Mufumbu imejengewa madarasa manne, mabweni mawili na matundu sita ya vyoo kwa gharama ya Sh milioni 352,huku Shule za Dr Salmin na Mwankonko kila moja ikiwa imejengewa madarasa mawili, mabweni mawili na matundu 10 ya vyoo, zikitumia Sh milioni 313 kila moja.

Katika Shule hizo miundombinu yote imekamilika na Halmashauri ipo tayari kuwapokea wanafunzi hao ambapo ongezeko hilo linafikisha shule za kidato cha tano na sita kuwa sita katika Manispaa ya Singida huku Mandewa Sekondari ikiwa shule pekee ya wasichana.
Ikumbukwe kuwa hizi ni juhudi za Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Dkt. Samia Suluhu Hassan ,Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye ameendelea kuboresha miundombinu ya elimu na kuhakikisha watoto wa kitanzania wapata elimu bora katika maeneo yao.