Sehemu ya taarifa ya hali ya Maendeleo kwa mkoa wa Shinyanga iliyosomwa na mkuu wa Mkoa Mh.Christina Mndeme Mbele ya waziri wa Tamisemi Mh.Mohamed Mchengerwa inaeleza kwamba kumekuwa na ongezeko la ukusanyaji wa maduhuli ya mapato ya serikali kutoka bilioni 22.39 mwaka 2021|2022 hadi kufikia kiasi cha shilingi bilioni 31.26 kwa kipindi cha mwaka 2022|2023.
Ambapo pia Jumla ya magari mapya 528 yamenunuliwa kwa lengo la kuhudumia watanzania katika sekta ya afya tangu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan alipoingia madarakani mnamo mwezi Machi mwaka 2021.
Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Tawala za mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI), Mohamed Mchengerwa ameyasema hayo Desemba 14 mwaka huu wakati akikabidhi magari ya usimamizi kwa sekta ya Afya mkoani Shinyanga na kufafanua mgawanyo wa magari hayo.
Naye Mbunge wa Jimbo la Msalala Mhe.Iddi Kassim Iddi ameeleza kwamba licha ya Halmashauri ya Msalala kujenga vituo vinne vya afya,kupokea vifaa tiba na kujenga zahanati 24,zahanati 7 pekee ndizo zilizofunguliwa kutokana na uhaba wa watumishi na kueleza kwamba nyasi zimeanza kuota katika zahanati ambazo hazifanyi kazi.
Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Ushetu Mh. Emmanuel Cherehani pia ameeleza kwamba changamoto ya watumishi ni changamoto kubwa sana katika jimbo lake kutokana na Jografia ya Jimbo hilo ilivyo.


