Na Eunice Kanumba – Shinyanga.
Tuanze kwa kulingazia jimbo la Solwa ambapo Mbunge aliyemaliza muda wake, Ahmed Ally Salum, ameongoza kwa kishindo katika kura za maoni za Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Shinyanga Vijijini, kwa nafasi ya ubunge wa Jimbo la Solwa, akijizolea kura 3,862 kati ya kura 7012 zilizopigwa na hakuna kura iliyoharibika.
Ahmed Salum alikuwa anachuana na wagombea wengine sita akiwemo Sosthenes Julius Katwale aliyeshika nafasi ya pili kwa kupata kura 2,288, akifuatiwa na Selemani Emmanuel Chokala (kura 645), Zinguji Mayala Machwele (kura 67), Alphistone Michael Bushi (kura 61), Costantine Joseph Budaga (kura 59) na Leonard Nduta Lukanya aliyepata kura 30.
Akizungumza baada ya kutangaza matokeo hayo, Katibu wa CCM Wilaya ya Shinyanga Vijijini ambaye pia ni Mkurugenzi wa Uchaguzi, Erenestina Richard amesema kuwa matokeo hayo ni ya awali, na uteuzi rasmi wa mgombea wa CCM bado unasubiriwa kupitia vikao vya juu vya uteuzi vya chama.
“Kuongoza katika kura za maoni siyo ushindi wala siyo kuwa umeteuliwa kuwa mgombea. Tunawaomba wagombea wote wawe watulivu na kusubiri maamuzi ya vikao vya uteuzi vya chama,” amesema.
Kwa upande wa jimbo jipya la Itwangi Kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Mbunge wa zamani wa Viti Maalum Mkoa wa Shinyanga, Azza Hillal Hamad, ameongoza katika kura za maoni za CCM Wilaya ya Shinyanga Vijijini, kwa nafasi ya ubunge wa Jimbo Jipya la Itwangi, akipata kura 2,630 kati ya kura 5,580 zilizopigwa.
Kura halali zilikuwa 5551 na kura zilizoharibika ni 29.
Azza Hillal ambaye amewahi kulitumikia Bunge kwa kipindi cha miaka 10 kupitia nafasi ya Viti Maalum, alikuwa anachuana vikali na wagombea wengine saba akiwemo John Elias Ntalimbo aliyeshika nafasi ya pili kwa kupata kura 2,322.
Wagombea wengine waliopata kura ni: Sebastian Pastory Malunde (kura 377), Fred Romanus Sanga (kura 122), Chrispine Myeke Simon (kura 45), Christian Misobi Budoya (kura 28), Anna James Ng’wagi (kura 16), na Hellena Daudi Mbuli aliyepata kura 11.
Akitangaza matokeo hayo, Katibu wa CCM Wilaya ya Shinyanga Vijijini na Mkurugenzi wa Uchaguzi, Erenestina Richard, amesema kuwa matokeo haya ni ya awali, na uteuzi wa mwisho wa mgombea wa CCM utafanywa na vikao vya juu vya chama.
“Kuongoza katika kura za maoni siyo ushindi wala siyo kuwa umeteuliwa kuwa mgombea.Tunawaomba wagombea wote wawe watulivu na wasubiri kwa subira maamuzi ya vikao vya uteuzi vya chama,” amesema.
Jimbo la Itwangi ni miongoni mwa majimbo mapya yaliyoundwa kuelekea Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025, likiwa limezua mvuto mkubwa kwa wananchi, wanachama na wapiga kura wa CCM katika mkoa wa Shinyanga.
Kwa upande wa jimbo la Kishapu jumla ya kura zilizopigwa zilikuwa 18443, huku kura 201 zikiharibika na kupelekea kura halali kusalia 12864, ambapo Lucy Mayenga ameibuka kidedea katika jimbo hilo kwa kupata kura 7814 akifatiwa na Bonda Nkinga aliyepata kura 1730 huku mbunge aliyemaliza muda wake Boniphase Butondo akiibuka na kura 1290.
Wengine ni Doto Kwigema aliyepata kura 597, George Jimisha kura 590, Madaha Chaba kura 503 huku John Ngano akipata kura 432.



One response to “SHINYANGA: MATOKEO NAFASI ZA KUGOMBEA UBUNGE CCM YAENDELEA KUWEKWA HADHARANI”
Can you tell uss more about this? I’d want to find out some additionsl
information. http://boyarka-Inform.com/