Katibu wa Shura ya Maimamu Tanzania, Sheikh Ponda Issa Ponda, leo Juni 5, 2025 amejiunga rasmi kuwa mwanachama wa Chama cha ACT Wazalendo.
Hafla hiyo, imefanyika Makao Makuu ya Chama hicho yaliyopo Magomeni, jijini Dar es Salaam mbele ya Viongozi mbalimbali wakiongozwa na Katibu Mkuu wa ACT – Wazalendo, Ado Shaibu.

“Nimeamua kujiunga na ACT Wazalendo kwa sababu ninayaona matumaini ya kweli ya mabadiliko ndani ya chama hiki. Tunahitaji siasa zenye maadili, zinazojali watu na zinazoweka mbele maslahi ya umma, si maslahi binafsi ya wachache,” alisema Sheikh Ponda.





