Mashambulio ya kijeshi nchini Iran, yaliyotekelezwa na jeshi la Marekani na Israel, yamesababisha vifo vya Wanafunzi 165 waliokuwa shuleni katika mji wa Minab uliopo Kusini mwa Taifa hilo.
Shambulio hilo, lilitekelezwa katika shule ya Shajareh Tayyebeh, eleo ambalo pia ni makazi ya kambi ya Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Iran.

Wakati huo huo, Jeshi la Israeli linaendelea na zoezi la kuwaokoa watu waliothriwa na makombora katika Mji wa Beit Shemesh ambapo zaidi ya watu 9 waliuawa na 51 kujeruhiwa.
Wachambuzi wa masuala ya vita wanasema hatua ya Israeli kuanzisha mashambulizi ni kujiweka kwenye mazingira hatari, kwa sababu Iran itaendelea kuwarushia makombora.