SHAMBA LA BANGI LATEKETEZWA GEITA, SERIKALI YATOA TAMKO

Na Ibrahim Rojala – Geita.

Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilayani Geita ikiongozwa na Mwakilishi wa Mkuu wa wilaya ya Geita, Lucy Beda pamoja na Wakala wa Huduma za Misitu Shamba la Miti Geita Lwamgasa, wameteketeza Hekari 3 na Nusu za shamba la Bangi iliyokuwa imelimwa katika Hifadhi ya Shamba la Miti Geita Lwamgasa.

Akizungumza na Waandishi wa Habari mara baada ya kuteketeza bangi hiyo, Mwakilishi wa Mkuu wa wilaya ya Geita ambaye pia ni katibu Tawala wa wilaya ya Geita, Lucy Beda amewataka baadhi ya wananchi wanaolima Bangi hiyo kuacha mara moja na badala yake wawekeze nguvu katika Kilimo kinachostaili katika maeneo hayo.

“Leo tulifika hapa kwenye shamba la Miti la Geita Lwamgasa ambalo kama tulivyoambiwa lina Hekari 28160 na eneo hili lililolimwa bangi lina Hekari tatu na nusu , tunafahamu wote kwamba hii ni hifadhi na kazi yake ni kuhifadhi miti kwa ajili ya kizazi chetu na kizazi kijacho, lakini tumeona wananchi wanaingia kwenye Hifadhi hii wanafanya shughuli za kibinadamu ikiwepo kuchungia mifugo pamoja na Kilimo,’ amesema.

Mhifadhi Mkuu wa Shamba la Miti Geita Lwamgasa, Aloyce Paschal amesema katika Msako wa kulibaini shamba hilo linalolimwa Bangi katika Hifadhi ya Shamba la Miti Geita Lwamgasa wamebahatika kumkamata mtuhumiwa huyo ambaye wamemfikisha katika Vyombo vya Sheria huku wakiimiza Jamii kuacha tabia ya kulima Bangi katika Maeneo yoyote yale ya Hifadhi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *