Categories

Do you have a Story?

Call us on 0677 644 444 to submit your news story or incident report!

Shabiki wa Yanga auwawa

Jeshi la Polisi Wilaya ya Geita linawashikilia walinzi watatu wa Kampuni ya Samike Security Campany kwa tuhuma za Kumpiga kwa kutumia rungu na kumuua Mfanyabiashara na Shabiki maarufu wa Yanga Alex Mayaya baada ya kumhisi ni Mwizi .

Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Geita, Safia Jongo amethibitisha kutokea kwa mauaji hayo huku akisema chanzo ni Walinzi hao kujichukulia sheria mkononi.

Kamanda Jongo amesema Baada ya ushindi wa Yanga dhidi ya Simba Alex alishangilia na kunywa pombe kupita kiasi kisha akaenda kwenye duka lake lililopo eneo la Kilimahewa Katoro Wilaya ya Geita akafungua duka na kutoa matairi mawili ya pikipiki ambayo alikuwa anauza na kwa bahati mbaya duka lake lile linaendeshwa na Kijana wake hvyo Walinzi hawamfahamu vizuri wakahisi ni Mwizi na kumkamata wakamshambulia kwa kumpiga na rungu.

Jongo ameongeza kuwa Baada ya kumpiga Mfanyabiashara huyo Walinzi hawakumpeleka Kituo cha Polisi bali walikaa naye mpaka asubuhi kulipokucha huku hali yake ikiwa mbaya na kupelekea umauti wake baada ya kumfikisha Hospitali kwa matibabu zaidi asubuhi.

Endelea kutufuatilia zaidi kupitia Instagram: @jambofmtz Facebook: @JamboFmRadioTZ Twitter: @jambofmtz TikTok: @jambofmtz_ Youtube: @jambofmtz Sikiliza LIVE: www.jambofm.co.tz Tembelea www.jambogroup.co.tz #jambofmtz #shinyanga #jambotanzania #kahama #tanzania #Utamu #Mwanafamilia #JamboGroup #yanga

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *