Naibu Katibu Mkuu anayeshughulikia Miundombinu Ofisi ya Rais – TAMISEMI Mhandisi Rogatus Mativila ametoa maelekezo kwa Sekretarieti za Mikoa, Serikali za Mitaa na Wadau mbalimbali kuwa kila ngazi ya utekelezaji wa usimamizi wa elimumsingi kuweka utaratibu wa kuandaa mpango kazi wa upatikanaji wa huduma ya chakula na lishe shuleni.
Mhandisi Mativila ameyasema hayo kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais – TAMISEMI Mohamed Mchengerwa katika uzinduzi wa Mpango wa Utekelezaji wa Mwongozo wa Kitaifa wa utoaji wa huduma ya chakula na lishe kwa wanafunzi wa elimumsingi.
Aidha, Mhandisi Mativila amesema Serikali na Wadau wa elimu watashirikiana katika utekelezaji wa huduma ya chakula na lishe shuleni ili kutoa huduma za kuwezesha shule kupata stoo za kuhifadhi chakula, majiko ya kupikia, mabwalo ya chakula, nishati na kuhakikisha baadhi ya shule ambazo hazijaanza kutoa huduma ya chakula hiyo zifanye hivyo.