SERIKALI YAWEKA MKAKATI KUKABILIANA NA JANGA LA UDUMAVU KATAVI

Na Daniel Gahu – Katavi.

Mkuu wa Mkoa wa Katavi, Mwanamvua Mrindoko ameongoza kikao kazi kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ofisi ya Mkuu wa mkoa kilichowakutanisha wakuu wa wilaya, wakuu wa taasisi mbalimbali za umma na zisizo za umma kujadili namna bora yakuwawezesha wananchi kupata lishe bora ili kuepukana na janga la udumavu.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa kikao hicho amesema kuwa kutokana na mkataba wa lishe wa kitaifa wa lishe bora Kwa wananchi lakini kama mkoa wa Katavi pekeake unao mpango mkakati wa ziada wakuhusiana na upatikanaji wa lishe Kwa wananchi hii ni kutokana na mkoa wa Katavi kukabiliwa na janga la udumavu hasa Kwa watoto hivyo imewapasa kuhakikisha chakula chote kinachozalishwa kinakuwa na kiini lishe kinachohitajika.

Aidha amesema kuwa ndani ya mkoa wa Katavi Kuna jumla ya mashine takribani 359 ambazo zinafungasha unga wa mahindi na 15 zinazo ongeza virutubishi kwenye unga ambazo ni sawa na asilimia 73 ya mashine zote.

Amessma, licha ya jitihada zinazochukuliwa na Serikali bado mwitikio wa wananchi juu ya matumizi ya vyakula vilivyoongezwa virutubishi ni mdogo sambamba na changamoto ya usimamizi hafifu Kwa viongozi wa halmashauri na ndio maana viongozi wote mko hapa ili kuongezewa uelewa ili kwenda kubadili fikra na uelewa Kwa wananchi juu ya matumizi lishe.

Kwa upande wake Afisa wa Biashara na Viwanda, Festo kapela nae amebainisha kuwa wizara imeshakwisha kusaini kanuni za urutubishi wa chakula za mwaka 2024 na zimeshazinduliwa rasmi mwezi machi mwaka huu mkoani Ruvuma, hivyo Sasa wanakwenda kuwapitisha viongozi wote wa halmashauri na ngazi ya mkoani ili waweze kusimamia kwa mafanikio na kuepukana na janga la udumavu nchini.

Akiendelea kuzungumza afisa huyo amesema kuwa, Wizara ya afya imenunua mashine (doze fire) 100 zakuongeza virutubishi katika unga wa mahindi ambapo mashine hizo zitagawiwa Kwa mikoa mitano.

Kila mkoa umepata mashine ishirini ikiwemo mkoa wa Katavi na mashine hizo zitakwenda Moja Kwa Moja katika jamii ili kumhudumia hata mtu mmoja mmoja anayekwenda kusaga debe moja naye aweze kupata virutubishi vinavyohitajika katika afya.

Nao wadhamini wa kikao hicho wakiongozwa na bwana Patrick Mafunda ambae ni afisa urutubishaji kutoka kampuni ya Tecno save amesema kuwa wataendelea kudhamini mikutano hiyo ili zoezi la urutubishaji wa vyakula linakwenda kama ilivyokusudiwa Kwa wasindikaji wa unga, mafuta na ngano pasipo kuingia gharama yoyote Kwa kutoa wataalamu wa usindikaji na kufikia viwango vinavyotakiwa na shirika la viwango nchini TBS.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *