Categories

Do you have a Story?

Call us on 0677 644 444 to submit your news story or incident report!

Serikali Yatoa Onyo Kwa Watumishi Wanaokikua Maadili Ya Kazi.

Na Gideon Gregory

Serikali imeonya ukiukwaji wa maadili kwa watumishi wa umma ikiwemo viashiria vya mapenzi ya jinsia moja na mavazi yasiyofaa kwa watumishi wa umma jambo ambalo limekuwa likichafua taswira ya serikali.


Hayo yameelezwa jijini Dodoma na Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bw. Xavier Daudi,wakati akifungua kikao kazi cha kubadilishana uzoefu kuhusu masuala ya maadili na utawala bora baina ya taasisi simamizi za maadili ya utendaji na mamlaka simamizi za maadili ya kitaluma.


Bw.Daudi amesema kuwa Ofisi imeanza kupokea tuhuma na malalamiko kuhusu kuwepo kwa viashiria vya mmomonyoko wa Maadili kinyume na mila na desturi za nchi yetu vinavyohusu vitendo vya mapenzi ya jinsia moja kwa baadhi ya watumishi wa umma.


Ameongeza kuwa, vitendo hivyo ni miongoni mwa vitendo vya kijinai kwa mujibu wa sheria za nchi lakini pia ni kinyume na maadili kwa mujibu wa miongozo ya utumishi wa umma.


“Hivyo, tumieni kikao kazi hiki, kujadili na kubadilishana uzoefu ili kuja na mapendekezo ya namna sahihi ya kudhibiti vitendo hivi na namna sahihi ya kushughulikia masuala haya yatakapojitokeza katika maeneo yenu ya kazi kwa baadhi ya watumishi wanaohusishwa navyo ili kuepuka kuchafua taswira ya utumishi wa umma kwa ujumla,”amesema Bw.Daudi


Aidha Bw.Daudi ameziomba taasisi za Dini kote nchini kusimamia maadili, kuonya na kukemea vitendo hivyo vya ndoa ya jinsia moja katika jamii ya kitanzania kwakuwa wana nguvu na Sauti kubwa ya kusikika zaidi.


“Hivi sasa zipo nchi zimeacha kuzaliana kutokana na kushamiri kwa vitendo hivyo vya mapenzi ya jinsia moja,Tanzania hatutaki kufika huko ndio mana tunakemea,”amesema Bw.Daudi


Kuhusu mavazi yasiofaa ameelekeza watumie waraka namba 6 wa utumishi wa umma unaozungumzia mavazi kuchukua hatua dhidi ya watumishi wanaochafua taswira ya serikali kwa kuvaa hovyo ndani na nje ya utumishi na kuongeza kuwa zipo taasisi ambazo viongozi wake wameanza kulegalega kwa kutochukua hatua na kuacha watumishi wakivaa mavazi kinyume cha maadili ya utumishi wa umma.


Aidha amewataka Watumishi wa umma wa kada za afya na ardhi kuachana na vitendo vilivyo kinyume na maadilii ya taaluma zao ikiwemo rushwa na kuwajibu vibaya wananchi wakati wa utoaji wa huduma kwani kumekuwepo na taarifa za malalamiko mengi kutoka vyanzo mbalimbali, yatokanayo na vitendo vya ukikuwaji wa maadili ya utendaji na maadili ya kitaaluma katika utumishi wa umma.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *