Serikali imeahidi kuendelea kuboresha mazingira ya ufanyaji biashara kwa kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili wawekezaji na wafanyabiashara nchini.
Hayo yameelezwa na Waziri wa Viwanda na Biashara, Dk. ashatukijaji alipokutana wafanyabiashara pamoja na wajasiriamali wa Mkoa wa Dodoma kwa ajili ya kuwasikiliza pamoja na kutatua changamoto zinawazowakabili.
Dk. Kijaji amesema kuwa tangu kuanza kutekelezwa kwa Mpango wa Kuboresha Mazingira ya Biashara hapa nchini (Blue Print), Serikali imefanikiwa kuondoa kodi, tozo na ushuru mbalimbali 374 kati ya 380.
Dk. Kijaji pia ameagiza kitabu kinachoainisha kodi hizo zilizoondolewa kichapishwe ndani ya wiki moja na kifikishwe kwa Wakuu wa Mikoa ili wafanyabiashara pamoja na wajasiriamali wajue kodi zipi zilizoondolewa kupunguza migogoro kati ya

Vile vile imeongeza kuwa katika kuendelea kuboresha mazingira ya ufanyaji biashara nchini, Serikali kupitia Wizara ya Viwanda na Biashara inatarajia kuanza kutoa leseni zote kupitia Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA).
Awali Leseni Daraja A zilizikuwa zikitolewa na Wakala huo na Leseni Daraja B zilikuwa zikitolewa na Halmashauri nchini hali iliyokuwa ikilalamikiwa na wafanyabiashara kote nchini kuwepo kwa urasimu pindi wanapo safirisha bidhaa au mazao kutoka halmashauri moja kwenda nyingine.
Hayo yameelezwa na Waziri wa Viwanda na Biashara, Dk. Ashatu Kijaji alipokutana wafanyabiashara pamoja na wajasiriamali wa Mkoa wa Dodoma kwa ajili ya kuwasikiliza pamoja na kutatua changamoto zinawazowakabili.
Waziri Kijaji amesema kuwa awali Halmashauri zilipewa mamlaka hiyo ya kukata leseni za biashara kutokana na mifumo ya upatikanaji wa leseni zamani ilikuwa ni lazima mfanyabiashara asafiri kwenda Dar es Salaam kwa ajili ya kupata leseni ya biashara lakini kwa sababu ya maendeleo ya Sayansi na Teknolojia wananchi hawana sababu tena ya kusafiri kwenda Dar Es Salaam kwa ajili kupata leseni ya biashara.