Serikali Yalaani Tuki la Kushambuliwa Mtoto Mwenye Ualbino Geita

Na Gideone Gregory,Geita

Siku chache baada ya kutokea kwa tukio la mtoto Julius Kazungu mwenye umri wa miaka 10 mwenye ulemavu wa ngozi (ualbino), Mkazi wa mtaa wa Mtakuja kata ya Katoro wilaya na Mkoa wa Geita kujeruhiwa kwa kukatwa na mapanga sehemu mbalimbali za mwili wake na mtu asiyejulikana,serikali imetoa tamko la kulaani tukio hilo.

Tamko hilo limetolewa na Naibu Waziri wa ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu Ummy Nderiananga wakati akizungumza na wananchi wa Mtaa wa Mtakuja  kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye ulemavu ambapo amesema serikali inalaani tukio hilo na kueleza kwamba wale wote waliohusika na tukio watasakwa na kuwajibishwa na kuameahidi kuwa Serikali itamsomesha mtoto huyo.

Nderiananga amesema pia baada ya tukio hilo, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewaagiza Wakuu wa Mikoa na Wakuu wa Wilaya Nchini kuwasaka na kuwakamata watu wanaoshambulia watu wenye ualbino nchini.

Nae Mwenyekiti wa chama cha watu wenye ualbino Tanzania Godson Mollel ameiomba serkali kuwalinda watu wenye ulemavu dhidi ya matukio ya kuvamiwa na kushambuliwa ili kuondoa hofu nchini juu ya maisha yao.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *