SERIKALI YATOA UFAFANUZI PAMBA JIJI FC KUFANYA MAZOEZI GIZANI

Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Hassan Mabuye ametoa ufafanuzi wa taarifa inayosambaa mitandaoni ikionesha wachezaji wa timu ya Pamba Jiji FC wakifanya mazoezi gizani, katika uwanja wa Benjamin Mkapa jini Dar es Salaam.

Katika taarifa yake kwa Umma, Mabuye ameeleza kuwa, Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo inaufahamisha umma kuwa, timu hiyo ilifika katika uwanja huo bila taarifa rasmi ya kuja kufanya mazoezi ya kujiandaa na mchezo wao dhidi ya timu ya Yanga SC wa
Septemba 24, 2025.

“Kwa kuwa Timu haikuwa imetoa taarifa mapema, baada ya kuwasili katika uwanja
huo majira ya saa 12:35 jioni wataalamu wa umeme uwanjani hapo walikuwa
wameshaondoka, hivyo ikalazimu kuwarudisha kazini na kufanikiwa kuwasha taa za uwanja huo saa 1:08 usiku,” ilieleza sehemu ya taarifa hiyo.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *