SERIKALI YAENDELEA NA USANIFU UJENZI MWAMALA A NA MWAMALA B SHINYANGA…

Na Gideon Gregory,  Dodoma. 

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Dkt. Festo Dugange amesema Serikali inaendelea na usanifu wa ujenzi wa daraja katika barabara Mwamala A-Mwamala B zilizopo Wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga ambalo awali liliathiriwa na mvua za Elninyo. 

Dkt. Dugange ameyasema hayo leo Bungeni hapa Jijini Dodoma wakati akijibu swali la Mbunge wa Kishapu Boniphace Butondo aliyehoji ni lini Serikali itapeleka fedha za dharura Wilayani humo ili kufanya matengenezo ya Barabara zilizoharibiwa na mvua za Elninyo Mwaka 2023/24.

“Wakala ya Barabara za Vijijini na Mijini Tanzania Wilaya ya Kishapu inao mtandao wa barabara wenye urefu wa kilomita 1024.66 ambapo kilomita 2 ni barabara za Lami, kilomita 405.64 ni barabara za changarawe na kilomita 617.02 (km 617.02) ni barabara za udongo,”amesema. 

Aidha, amesema katika mwaka 2023/24, Serikali ilifanya tathmini ya mtandao mzima wa barabara katika Wilaya hiyo ili kubaini ukubwa wa uharibifu ambapo jumla ya shilingi Bilioni 2.5 zinahitajika ili kuzifanyia matengenezo barabara hizo. 

Pia ameongeza kuwa katika kukabiliana na changamoto hiyo, Serikali ilipeleka shilingi Milioni 190 katika mwaka 2023/24 kwa ajili ya kufanya matengenezo ya dharura kwa baaadhi ya maeneo na tayari yamefanyiwa kazi ikiwemo barabara ya Mwamakanga-Mwanghiri kilomita 4.5 na makalavati 7. 

“Serikali itaendelea kuzifanyia matengenezo barabara zilizoathiriwa na mvua kulingana na upatikanaji wa fedha,” – ameongeza. 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *