Serikali Yabuni Migahawa Inayotembea

Ili kuendelea kuongeza wigo wa masoko, kuongeza mauzo ya kahawa katika soko la ndani kutoka asilimia 7% hadi asilimia 15% ya kahawa yote inayozalishwa Nchini, Serikali imeendelea kubuni na kutengeneza migahawa inayotembea kwa kutumia pikipiki za miguu mitatu zitakazotumika katika uuzaji wa kahawa katika maeneo mbalimbali ya Umma na kwenye mikusanyiko ya watu.

Hayo yameelezwa leo Aprili 30,2024 Bungeni Jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Kilimo David Silinde wakati akijibu swali la Mbunge wa Vwawa,Japhet Hasunga aliyetaka kujua mkakati mahsusi wa Serikali wa kutafuta masoko ya zao la Kahawa.

Silinde amesema mkakati mwingine ni imeweka mazingira mazuri ya biashara ili kuvutia uwekezaji kwenye viwanda vya kuongeza thamani yaliyopelekea ongezeko la viwanda kutoka 21 hadi kufikia viwanda 37 vilivyopo sasa.

“Kuongeza kodi kwa bidhaa za kahawa zinazotoka nje ya nchi kutoka asilimia 25 mpaka 35 ya thamani ya kahawa, kuondoa kodi kwenye vifungashio vya kahawa ambavyo kwa kiasi kikubwa vinapatikana nje ya nchi,”amesema.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *