Categories

Do you have a Story?

Call us on 0677 644 444 to submit your news story or incident report!

Serikali ya kamilisha maandalizi ya kidato cha kwanza

Serikali imesema imekamilisha maandalizi ya miundombinu ya kuwapokea wanafunzi wote watakaokwenda kidato cha kwanza katika mwaka ujao wa masomo.

Hayo yamesemwa na Rais Samia Suluhu Hassan Kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa twitter wakati akiwatakia heri ya mtihani watahiniwa wa darasa la saba walioanza mtihani wao wa darasa la saba leo.

Jumla ya watahiniwa 1,397,370 wanafanya mtihani huo leo Jumatano na kesho alhamis ambapo kati yao wavulana ni 654,652 sawa na asilimia 46.85 na wasichana 742,718 sawa na asilimia 53.15.

“Nawatakia kila la kheri wanafunzi wote wa darasa la saba wanaoanza mitihani yao ya kuhitimu leo. Mmefikia hatua muhimu ya safari yenu ya awali, kuelekea njia mtakazochagua siku za usoni katika kutoa mchango wenu kusukumu mbele gurudumu la maendeleo ya Taifa letu.

“Serikali tayari imekamilisha maandalizi ya miundombinu ya kuwapokea wote mtakaoendelea na kidato cha kwanza mwaka 2024,” ameandika Rais Samia.

“Nawaombea kwa Mwenyezi Mungu alivewasimamia toka mwanzo wa safari hii ya elimu hadi sasa, akawape utulivu na afya njema, ili mfanye vizuri mitihani yenu,”amesema.

Jumla ya watahiniwa 1,397,370 wanafanya mtihani huo leo Jumatano na kesho alhamis ambapo kati yao wavulana ni 654,652 sawa na asilimia 46.85 na wasichana 742,718 sawa na asilimia 53.15.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *