Serikali imesema ina mpango wa kuboresha soko la matunda lililopo katika kata ya Kambarage katika Halmashauri Ya Manispaa Ya Shinyanga kwa kuvunja soko lililopo ambalo ni chakavu na kujenga la kisasa lenye miundo mbinu rafiki ya ufanyaji biashara ikiwemo umeme na mitaro ya kutiririsha maji huku suala la usafi likihimizwa na kufanywa kuwa kuwa tabia na mazoea kwani eneo la soko lazima liwe safi ili kuzuia magonjwa ya kuambukiza.

Hayo yamesemwa leo na mkuu wa wilaya ya Shinyanga Johari Samizi wakati akijibu changamoto mbalimbali zinazowakabili wafanyabiashara katika soko Hilo katika maadhimisho ya siku ya usafi duniani ambayo kwa Manispaa Ya Shinyanga yamefanyika leo katika soko hilo lengo ili kuhimiza usafi katika maeneo ya kazi kwa wafanyabiashara hao.
Naye afisa mipango wa halimashauri ya Manispaa Ya Shinyanga Menisalia Mrema amekiri kuwa soko hilo lina chnagamoto nyingi tofauti na masoko mengime yaliyopo katika Manispaa Ya Shinyanga likiwemo suala la ubovu wa miundo mbinu mbalimbali hivyo soko hilo litajengwa kwa msaada wa Benki ya dunia na tayari limeingizwa katika mpango wa bajeti ya mwaka wa fedha 2023/2024.
Awali baadhi ya wafanyabiashara katika soko hilo wameeleza changamoto mbalimbali zinazowakabili na kupelekea kukosa mazingira rafiki ya ufanyaji wa biashara huku wakiimba serikali iwasaidie kumaliza changamoto hizo.
Kila mwaka September 15 Tanzania huungana na nchi nyingine 150 duniani kuadhimisha siku ya usafi duniani kwa lengo la kupinga tatizo la uchafu katika mitaa mbalimbali.