
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mohamed Mchengerwa, amesema mwezi ujao serikali inatarajia kutangaza nafasi za kazi 25,000 kwenye sekta za afya na elimu ili kukabiliana na upungufu wa watumishi uliopo.
Katika ziara yake ya kukagua miradi na kuongea na watumishi mkoani Simiyu, Mchengerwa, amesema kuwa baada ya kukamilisha taratibu za serikali, mkoa huo utaongezwa watumishi walioombwa kwenye kada mbalimbali zikiwamo afya na elimu.
“Ukishikwa shikilia, ukipata nafasi ishikilie kama hamwamini angalieni tuliokuwa nao serikalini huko, nje hali zao zikoje, mkiweka kipimo hicho mtajiongeza kuwa kuna uhitaji wa kuwahudumia watanzania wenye nchi yao, asije pale ukamfokea ukashindwa kumhudumia,” alionya.
One response to “Serikali kutangaza ajira 25, 000 januari 2024”
That is good ila watuangalie walimu jamani wazazi wanakata tamaa tumesoma ajira hatupati Hadi miaka 8sasa Tangu nimalize masomo ya shahada yangu ya ualimu