Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mohamed Mchengerwa ametangaza rasmi mkakati wa kukuza na kuendeleza wakandarasi wazawa ili wafikie viwango vya kimataifa vya ubora na usalama.
Mchengerwa ameyasema hayo Jijini Dodoma wakati wa kikao na watumishi wa Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) kilichofanyika Makao Makuu ya TARURA yaliyopo mji wa serikali Mtumba.
Kwa upande wake Meneja wa TARURA Mhandisi Victor Seff amesema kuwa agizo lililotolewa na Waziri Mchengerwa la kukuza wakandarasi wazawa wataenda kulifanyia kazi kwa kushirikiana na bodi ya makandarasi.