
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Hassan Abbasi amesema sekta ya utalii nchini kwa sasa imekua kwa kasi kutokana na mikakati ya kutangaza utalii hivyo kwa sasa wanategemea kuweka mazingira mazuri zaidi ya Kimiundombinu ili kuchagiza uwingi wa wageni kufika hifadhini hapo.

Akitembelea na kukagua ujenzi wa miundombinu mbalimbali hifadhini hapo, Dkt. Abas amesema ‘’ Kwa jiografia ya Mikumi hili ni eneo ambalo ndege nyingi zinatua hapa kutoka Zanzibar hivyo tunajenga uwanja mdogo lakini wa kisasa wa ndege, kuongeza malazi lakini tunakuja na mradi wa kujenga viwanja vya michezo na burudani ili watu wabarizi na kucheza ndani ya hifadhi huku wakiwaona wanyama huku na kule,”
