Serikali kujadili kuweka picha ya rais Samia kwenye fedha za Tanzania

Serikali imesema imeupokea na itaujadili ushauri wa kuweka kumbukumbu ya kudumu kwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hasssan kwa kuweka picha yake kwenye fedha za Tanzania ikiwa ni heshima ya kuwa na Rais wa kwanza Mwanamke anayefanya kazi nzuri na kutambua utendaji wake.

Waziri Mkuu wa Tanzania Kassim Majaliwa amesema hayo Bungeni Jijini Dodoma
leo wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum Vijana Ng’wasi Kamani aliyetaka kujua ni lini Serikali itaweka kumbukumbu ya kudumu ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuweka picha yake kwenye fedha za Nchi na kutambua mchango wa Rais wa kwanza Mwanamke Tanzania

Waziri Mkuu amesema Maamuzi ya kuweka picha kwenye noti mara nyingi yanafanywa na maamuzi ya Kiongozi mwenyewe kwa kushauriana na Benki Kuu na serikali inatambua kuwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ametoa mchango mkubwa katika Taifa  kwa hiyo suala hilo litajadiliwa pale ambapo litafanyiwa maamuzi kwa kushirikiana na Benki Kuu taarifa zitatolewa rasmi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *