
Serikali kupitia Wizara ya Afya imedhamiria kuimarisha na kuwekeza kwenye Afya za vijana balehe hasa katika hali za Lishe, Afya ya Akili pamoja na elimu ili kujikinga na magongwa yakuambukiza ikiwemo VVU/UKIMWI ikiwa ni kipaumbele cha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Waziri wa Afya Ummy Mwalimu amesema hayo wakati akifungua Kongamano la Tano la Kisayansi kuhusu masuala ya vijana balehe (15-19) lenye lengo la kujadili namna ya kubadili Tafiti za Afya kwa Vijana wa rika balehe na Lishe kuwa za vitendo.


